Illinois Early Intervention Clearinghouse

Matokeo: Kupima Mafanikio ya EI

Matokeo ya Familia
Kama sehemu ya ushiriki wako katika afua za awali, tutakusaidia kupata maarifa na stadi katika maeneo haya matatu muhimu:

  • Kujua haki zako
  • Kushirikisha mahitaji ya mtoto wako
  • Kuchukua hatua sahihi ili kukidhi mahitaji ya mtoto wako

Matokeo ya Mtoto
Ni muhimu kujua jinsi mtoto wako anavyokua kama matokeo ya kupewa huduma za afua za awali. Unamuona mtoto wako katika shughuli na mazingira ambayo wajumbe wengine wa timu hawamuoni. Matokeo matatu ya mtoto ni:

  • Kujenga mahusiano chanya ya kijamii
  • Kupata na kutumia maarifa na stadi
  • Kuchukua hatua sahihi ili kukidhi mahitaji yake

Matokeo Fanisi ya IFSP
Matokeo fanisi ni manufaa au matunda unayotaka kwa mtoto wako na familia yako kama matokeo ya kushiriki katika afua za awali. Matokeo haya yanatija katika maisha yako ya kila siku na yanawekwa katika mpango binafsi wa huduma kwa familia (IFSP) ambao uliuandaa pamoja na timu yako ya EI.

Una Jukumu Muhimu Katika Ukuaji wa Mtoto Wako
Kama mjumbe wa timu ya EI, ushiriki wako wa kivitendo ni muhimu kwa sababu wewe ndiye unayemjua vizuri zaidi mtoto wako. Unawezaje kusaidia?

  • Mchunguze mtoto wako ukiwa nyumbani na maeneo ya jumuiya
  • Shirikisha unachokijua kwa wajumbe wengine wa timu ya EI
  • Uliza timu yako ya EI ikiwa una maswali kuhusu mtoto wako
  • Jibu Maswali ya Utafiti wa Matokeo ya Familia

Title in English: Early Intervention Outcomes