Ni Wakati Gani wa Kuondoka Kwenye Programu ya EI?
Mtoto wako anaweza kuondoka kwenye programu ya EI baada ya ukuaji wake kuimarika na matokeo ya mtoto wako kuwa yamefikiwa. Vinginevyo, mtoto wako anaweza kubaki katika programu ya EI hadi afikishe miaka mitatu, au huduma za ziada zikiwa chaguo kwa mtoto. Angalau miezi sita kabla ya mtoto wako kufikisha miaka 3, wewe au timu yako ya IFSP mtaanza kupanga kuondoka kwenye huduma za EI. Hii itakupa muda wa kufahamu iwapo mtoto wako ana ustahiki wa huduma za elimu maalum ya utotoni (ECSE) kupitia wilaya mahalia ya shule au, kulingana na tarehe yake ya kuzaliwa, iwapo mtoto wako ana ustahiki wa huduma za ziada. Si watoto wote watakuwa na ustahiki wa ECSE, na mtoto wako anaweza kuhitaji kufanyiwa tathmini nyingine.
Kimsingi, ukiomba teknolojia saidizi lakini kuna chini ya miezi sita kabla ya mtoto wako kufikisha umri wa kuondoka kwenye afua za awali, mtoto wako anaweza kutopokea teknolojia saidizi kutoka afua za awali.
Hizi ni hatua husika na jukumu lako katika mchakato:
- Zungumza na mratibu wako wa huduma, msaidizi maalum wa wazazi, na watoa huduma za EI kuhusu namna ya kumwandaa mtoto na familia yako kwa ajili ya mpito. Mratibu wako wa huduma atakuuliza iwapo unataka kupewa rufaa kwenda wilaya mahalia ya shule kwa ajili ya huduma za ECSE. Unaweza kukubali au kukataa. Ukikubali, saini yako inahitajika ili kushirikisha taarifa kwa wilaya yako mahalia ya shule.
- Hudhuria mkutano wa kupanga kipindi cha mpito cha mtoto wako.
- Ikihitajika, shiriki katika tathmini za wilaya ya shule za mtoto wako.
- Pata uamuzi kuhusu ustahiki wa mtoto wako katika ECSE, huduma za ziada za EI, marekebisho, na huduma kutoka wilaya ya shule.
- Akiwa na ustahiki, weka mipango ya Mpango Binafsi wa Elimu (IEP) au mpango wa Section 504. Kama hana, fikiria rasilimali nyingine za jumuiya kwa mtoto wako.

