
Ukiwa na wasiwasi wowote kuhusu huduma, au usipokubaliana na maamuzi kuhusu mtoto wako, unapaswa kuzijadili na mratibu wako wa huduma katika CFC. Huduma hizi au maamuzi haya yanaweza kuhusiana na mambo kama utambuzi, upimaji, ufanyaji tathmini, uchaguliwaji, au 26 Programu ya Afua za Awali (EIP) Illinois: Mwongozo kwa Familia usahihi wa huduma. Usiporidhika na matokeo ya majadiliano, chaguzi rasmi za usuluhisho wa kiutawala zimeainishwa katika sheria. Hizi zinajumuisha:
- Malalamiko kwa jimbo. Unaweza kufungua lalamiko la maandishi, lililosainiwa, katika Idara ya Huduma za Binadamu Illinois (IDHS) ukidhani mtoa huduma amekiuka sheria au kanuni kuhusu Sehemu C ya Programu ya Afua za Awali. Maelezo lazima yajumuishe vielelezo vinavyothibitisha lalamiko lako. IDHS inaweza kutumia Programu ya Kufuatilia Afua za Awali Illinois (EIMP) kufanya uchunguzi (https://earlyinterventionmonitoring.org)
- IDHS ina siku 60 tangu kupokea lalamiko kuchunguza na kuandika uamuzi wake. Katika kipindi hiki, IDHS inaweza kufanya uchunguzi wa kujitegemea.
- Uamuzi wa IDHS lazima ujumuishe gunduzi kutokana na uchunguzi, matokeo, na sababu za kutoa uamuzi wa mwisho.
- Ikiwa lalamiko litagundulika kuwa la kweli au halali, basi uamuzi lazima ujumuishe taratibu za kusahihisha chanzo cha lalamiko.
- Upatanishi. Ikiwa kuna hali ya kutokukubaliana kati yako na mtoa huduma mahalia, CFC, au IDHS, unaweza kuomba upatanishi at DHS.BAH@illinois.gov. Upatanishi ni kikao cha hiari kinachosimamiwa na mpatanishi mwenye sifa katika eneo rahisi kwako ndani ya siku 10 baada ya kutoa ombi. Jukumu la mpatanishi ni kusaidia wahusika wasiokubaliana kuzungumza na kufikia mwafaka. Mpatanishi hawezi kulazimisha makubaliano. Majadiliano yanayofanyika wakati wa upatanishi ni siri. Upatanishi ni hiari, na unapaswa kukubali kwa uhuru kushiriki. Serikali ya jimbo inalipia gharama za upatanishi. Makubaliano ya upatanishi yanarekodi masharti yaliyokubaliwa. Huduma zilizokubaliwa hapo awali kwa mtoto wako zinapaswa kuendelea wakati wa kipindi cha upatanishi.
- Usikilizaji wa shauri la utaratibu wa haki. Unaweza kuomba usikilizaji wa shauri la taratibu za haki (due process hearing) ili kutatua lalamiko kwa mtoa huduma wako au CFC. Ukiomba usikilizaji wa shauri la taratibu za haki, wewe na CFC yako mna hadi siku 30 za kutatua lalamiko hadi uridhike. Usiporidhika, usikilizaji wa shauri la taratibu za haki utafanyika.
- Usikilizaji wa shauri la taratibu za haki ni sawa na kesi ya mahakamani.
- Usikilizaji huu lazima ufanyike kwa muda na mahali ambapo ni rahisi kwako.
- Afisa wa usikilizaji wa shauri atasikiliza pande zote za kutokubaliana. Afisa wa usikilizaji wa shauri hapaswi kuwa mwajiriwa wa shirika lolote au chombo kingine kinachotoa huduma za EI kwa mtoto wako.
- Wakati wa usikilizaji wa shauri, unaweza kuja na mwanasheria, wakili, au rafiki mwenye uelewa au mafunzo maalum kuhusu mtoto wako au kuhusu watoto wenye ulemavu.
- Una haki pia ya kuja na mtoto wako na kuruhusu usikilizaji wa shauri uwe wazi kwa umma.
- Ili kupata wakili, unaweza kuwasiliana na Equip for Equality, shirika la Mfumo wa Ulindaji na Utetezi Illinois https:// equipforequality.org/
- Una haki ya kupewa nakala ya rekodi za usikilizaji wa shauri, gunduzi, na maamuzi, bila gharama yoyote. Uamuzi kwa maandishi unapaswa kutumwa kwako ndani ya siku 45 baada ya kipindi cha usuluhisho cha siku 30 kumalizika. Upande ulioshindwa una haki ya kukata rufani dhidi ya uamuzi.

