
Katika kikao chenu cha kwanza mratibu wa huduma atakuelezea programu ya EI na kusaidia kuweka mipango ya upimaji na tathmini. Hii inaitwa kikao cha awali (intake meeting) kwa sababu utaombwa kushirikisha taarifa kuhusu mtoto wako na familia yako.
- Mratibu wa huduma atakuuliza maswali kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wako, historia ya kitiba, na shughuli zako za kila siku (muda wa kucheza, milo, ratiba ya kulala, ulezi wa mtoto, n.k.).
- Unaweza pia kupewa orodha maalum ya kubaini stadi na uwezo wa mtoto wako.
- Utaombwa kusaini fomu za ridhaa na kukubali kwamba mratibu wa huduma anaweza kushirikisha taarifa kuhusu mtoto wako kwa timu ambayo itampima na kumtathmini mtoto wako na inayoweza kukusaidia kupanga huduma za EI. Ukiridhia, basi mtoto wako anaweza kupewa rufaa ya kufanyiwa upimaji na tathmini.
- Mchakato huu ni bure kwa familia zote.
Hatua Inayofuata: Shiriki katika Upimaji na Tathmini

