Mapitio wa IFSP

Title in English: IFSP Review

IFSP inaweza kubadilishwa. Kadri mtoto wako anavyokua na kupiga hatua, mambo muhimu kwako yanaweza kubadilika, na hivyo kuhitaji huduma mpya au tofauti. Timu ya EI inaweza kubadilisha huduma ili kukidhi vizuri zaidi mahitaji ya mtoto na familia yako.

Wewe na timu yako ya IFSP mtapitia maendeleo ya mtoto kila baada ya miezi sita na kuboresha mpango angalau mara moja kwa mwaka. Mahitaji yako yakibadilika, wewe na timu yako mnaweza kukutana mara nyingi zaidi ili kuubadili mpango kadri itakavyohitajika. Dhumuni la mapitio ya IFSP ni kubaini iwapo mtoto wako anaendelea kuwa na ustahiki wa programu ya EI au iwapo mtoto wako amefikisha hatua muhimu za ukuaji na hivyo kutohitaji tena huduma.

Ili kujiandaa na mapitio ya IFSP, unaweza kujiuliza maswali haya yafuatayo:

  • Je, mtoto amepiga hatua?
  • Je, matokeo ya sasa yanahitaji huduma tofauti au za ziada?
  • Je, vipaumbele vya mtoto wako vimebadilika?
  • Je, huduma gani mtoto wako anaweza kuzihitaji siku za usoni?
  • Je, mtoto wako amefikisha matokeo ya IFSP? Je, matokeo mapya yanafaa?
  • Je, familia yako imefikisha matokeo ya IFSP? Je, matokeo mapya yanahitajika?

Hatua Inayofuata: Mpito

Title in English: IFSP Review