
Programu ya EI ya Illinois ilianzishwa na sheria ya jimbo ili kupatana na Sehemu C ya Sheria ya Elimu kwa Watu wenye Ulemavu (IDEA) ya serikali kuu. IDEA inaelezea haki zako kama mzazi wa mtoto anayepokea huduma za EI. Baadhi ya haki za uzazi zimeelezewa hapa kwa ufupi.
- Mnapaswa kufanya kikao cha kuandaa IFSP mapema iwezekanavyo ila isizidi siku 45 tangu mtoto wako kupewa rufaa kwenda programu ya EI.
- Huduma lazima zianze ndani ya siku 30 baada ya kusaini IFSP
- Unaweza kukubali, kukataa, au kusitisha huduma wakati wowote. Ushiriki wako ni hiari na unahitaji ridhaa yako ya maandishi. Mahitaji yako yakibadilika, wewe na timu yako mnaweza kukutana mara nyingi zaidi ili kuubadili mpango kadri itakavyohitajika.
- Ukihitaji mkalimani, utapewa mmoja atayekusaidia katika mchakato mzima wa EI. Huduma hii inatolewa bure. Nyaraka za karatasi ngumu zinaweza pia kutafsiriwa katika lugha yako ya asili kama zitahitajika. Omba mkalimani wakati utakapowasiliana na ofisi yako ya CFC.
- Ridhaa inamaanisha kwamba unatoa ruhusa ya wewe na mtoto wako kupokea huduma. Unaombwa kusaini waraka wa IFSP ili kuonesha kwamba unaelewa na kuukubali mpango husika na huduma zilizobainishwa ndani yake. Pia utaombwa kusaini ridhaa za kushirikisha taarifa kuhusu mtoto na familia yako kwa watoa huduma za afua za awali au mashirika mengine ambayo yanamhudumia mtoto na familia yako. Wewe na familia yako mnapojiandaa kuondoka programu ya EI, utaombwa kutoa ridhaa ya maandishi kabla rekodi zako kutolewa kwa wilaya eneo la shule au shirika lingine ambalo litamhudumia mtoto wako akifikisha miaka 3.
- Notisi Iliyoandikwa Kabla – Notisi ya maandishi lazima itolewe kwako kabla ya shirika la EI au mtoa huduma za EI kufanya badiliko katika huduma za EI za mtoto wako. Notisi lazima itolewe kwa lugha ya kawaida unayoitumia. Unapaswa kupokea notisi ya maandishi kuhusu kikao chochote, ili uwe na muda wa kutosha wa kufanya taratibu za kuhudhuria.
- Mapitio ya Rekodi – Una haki ya kupitia rekodi zozote zinazohusiana na huduma za EI za mtoto wako. Rekodi zinapaswa kupatikana kwako ndani ya siku 10 za kalenda baada ya kuziomba. Unaweza kuomba kurekebisha rekodi.
- Usiri wa Rekodi – Rekodi zote za huduma za EI za familia yako ni siri. Watoa huduma wako watashirikishana taarifa wao kwa wao ili kutoa huduma bora kwa familia yako. Rekodi zitashirikishwa tu kwa wengine kama inavyoruhusiwa na sheria za faragha k.m., Sheria ya Uhamishaji na Uwajibikaji wa Bima ya Afya (HIPAA) na Sheria ya Haki na Faragha ya Elimu ya Familia (FERPA).
Ukiwa na wasiwasi wowote kuhusu huduma, au usipokubaliana na maamuzi kuhusu mtoto wako, unapaswa kuzijadili na mratibu wako wa huduma katika CFC. Huduma hizi au maamuzi haya yanaweza kuhusiana na mambo kama utambuzi, upimaji, ufanyaji tathmini, uchaguliwaji, au 26 Programu ya Afua za Awali (EIP) Illinois: Mwongozo kwa Familia usahihi wa huduma. Usiporidhika na matokeo ya majadiliano, chaguzi rasmi za usuluhisho wa kiutawala zimeainishwa katika sheria.
Pata maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko.

