
Wewe ndiye unayemjua mtoto wako vizuri zaidi; unajua mtoto wako anachokipenda na asichokipenda. Uelewa wako huu unakufanya kuwa mshirika muhimu kwenye timu ya mtoto wako.
- Timu itajumuisha wewe, mratibu wa huduma, na angalau watoa huduma wengine wawili wa EI.
- Idadi ya wajumbe wa timu inaweza kutofautiana kulingana na mahitaji ya mtoto wako na inaweza kujumuisha wataalamu mbalimbali, kama vile tabibu wa ukuaji na tabibu maungo.
- Wajumbe wa timu watamchunguza na watahusiana na mtoto wako. Wanaweza kupima uwezo wa mtoto wako na kuulinganisha dhidi ya hatua muhimu za ukuaji. Wanaweza kumchunguza na kumhusisha mtoto wako katika shughuli ili kuona anachoweza kufanya na anachopenda kufanya.
- Ikiwa lugha yako ya asili si Kiingereza, programu ya EI itakupa mkalimani, kama atapatikana, kwa ajili ya upimaji na tathmini. Hutatozwa gharama yoyote kwa huduma ya mkalimani. Nyaraka za karatasi ngumu zinaweza pia kutafsiriwa katika lugha ya asili ya familia yako kama zitahitajika.
Timu itampima na kumtathmini mtoto wako katika maeneo yote matano ya ukuaji:
- Kimwili (jinsi mtoto wako anavyosonga na kuchunguza),
- Kiakili (jinsi mtoto wako anavyojifunza),
- Kuwasiliana (jinsi mtoto wako anavyokufahamisha kile anachohitaji),
- Kijamii na kihisia (jinsi mtoto wako anavyohusiana nawe na kuonesha hisia zake), na
- Kubadilika kulingana na mazingira (jinsi mtoto wakoanavyoshiriki shughuli za kila siku za kujijali).
Watakuuliza maswali kama vile:
- Je, mtoto wako anakua kwa namna unayotegemea akue?
- Je, una wasiwasi kuhusu ukuaji wa mtoto wako?
- Je, mtoto wako anafanya mambo tofauti na ndugu zake au watoto wengine unaowajua katika umri huu?
- Je, ratiba za familia yako zipoje, kama vile muda wa kuoga na kula?
- Je, mtoto wako ana mwitikio gani wakati wa shughuli za familia?
- Je, vipi ni vipaumbele vya familia yako kwa mtoto wenu?
- Je, unahitaji nini ili kuisaidia familia yako kuwa makini na vipaumbele hivyo?
Kumbuka hilo una haki ya kupata ripoti za tathmini.
Hatua Inayofuata: Kuamua Kustahiki

