Nini Kinampa Mtoto Wangu Ustahiki wa Huduma?

Mtoto wako mdogo (mchanga hadi miezi 36) ana ustahiki wa huduma kupitia programu ya EI Illinois ikiwa

  • ana uchelewaji wa 30% katika angalau eneo au nyanja moja ya ukuaji, au
  • ana ugonjwa unaojulikana kusababisha tatizo la uchelewaji wa kukua au ulemavu, au 
  • yupo katika hatari kubwa ya uchelewaji mkubwa wa kukua.

Sababu zifuatazo zinamfanya mtoto astahili kupokea huduma za msaada wa mapema kiotomatiki: 
– watoto wenye kiwango cha juu cha sumu ya risasi kwenye damu zaidi ya au sawa na kiasi cha maikrogramu 3.5 kwa desilita
– mtoto yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 3 ambaye amethibitishwa kuwa anadhulumiwa au hatunzwi vizuri kama inavyoelezwa katika Sheria ya Kitaifa ya Matibabu na Uzuiaji wa Dhuluma kwa Watoto na katika Sheria ya Illinois (325 ILCS 20/3)

pencils and paper tablets

Baada ya Utathmini 

  • Utaarifiwa na CFC kama mtoto wako ana ustahiki.
  • Ustahiki wa afua za awali haumaanishi moja kwa moja kwamba mtoto wako amethibitishwa rasmi kitiba kuwa na tatizo au ulemavu. Inaweza kumaanisha tu kwamba mtoto wako ana uchelewaji unaoweza kutibiwa na huduma zitolewazo na programu ya afua za awali.
  • Una haki ya kupata ripoti za tathmini.
  • Ikiwa mtoto wako ana ustahiki na ukaamua kwamba unataka kushiriki katika programu ya EI, basi kikao kitafanyika kati yako na timu yako ili kuandaa Mpango Binafsi wa Huduma kwa Familia (IFSP).
  • Uandaaji wa mpango ni bure na kikao cha IFSP lazima kifanyike ndani ya siku 45 baada ya mtoto wako kupewa rufaa kwenda programu ya EI.
  • Ingawa si lazima, unaweza kuomba matokeo ya tathmini kabla ya kikao. Hii inaweza kukusaidia kujiandaa kwa ajili ya kikao kwa kuisoma ripoti, kuandaa maswali ya kuiuliza timu, na kutoa maoni ya ziada.

Ikiwa mtoto wako hatakuwa na ustahiki, basi IFSP haitaandaliwa na hakuna huduma za EI zitakazotolewa. Mratibu wa huduma anaweza kukupa orodha ya rasilimali za jumuiya zinazoweza kukidhi mahitaji ya familia na ya mtoto wako. Ukiwa na wasiwasi mpya kuhusu ukuaji wa mtoto wako, unaweza kuwasiliana na ofisi ya CFC wakati wowote kabla ya mtoto wako kufikisha miaka 3 ili kujadili wasiwasi wako. 

Hatua Inayofuata: Andaa Mpango Binafsi wa Huduma kwa Familia