
Afua za awali huduma lazima zianze ndani ya siku 30 baada ya kusaini IFSP.
Huduma za EI zinapaswa kutolewa katika mazingira halisi ya mtoto. Hii inamaanisha mahali ambapo mtoto wako anatumia muda wake mwingi na ambapo watoto wengine wadogo wasio na ulemavu au tatizo la uchelewaji wa kukua wanapotumia muda wao mwingi. Mazingira halisi yanaweza kuwa nyumbani kwako, kituo cha ulezi wa watoto, maktaba, nyumbani kwa ndugu, au mahali kwingine ambapo kwa kawaida familia yako inatumia muda mwingi. Mazingira halisi hukuwezesha wewe na mtoa huduma ya EI kutumia ratiba zenu za kila siku kumfundisha mtoto wako stadi au tabia mpya. Shughuli hizi zikiweza kujumuishwa katika ratiba ya kila siku ya mtoto wako, wewe na walezi wengine mtaweza kuzifanya mara kwa mara zaidi na mtoto wako wakati mtoa huduma ya EI asipokuwepo.
Unaweza pia kupokea msaada kutoka kwa afisa wa ushirikiano na wazazi: mzazi wa mtoto ambaye tayari amepokea huduma za Mpango wa Msaada wa Mapema wa Illinois. Kama mtu ambaye amepitia hali unayopitia, mtu huyu hukusaidia kwa kusikiliza au kujibu maswali yako.
Huduma za EI zinaweza kujumuisha:
- Teknolojia saidizi (AT)
- Matibabu ya audiolojia/usikiaji
- Tiba ya ukuaji/mafunzo maalum
- Mafunzo na usaidizi kwa familia
- Ushauri wa kiafya
- Ukalimani na tafsiri katika lugha nyingine
- Huduma za kitiba (kwa madhumuni ya uchunguzi na upimaji tu)
- Uuguzi
- Lishe
- Tiba Vitendo (OT)
- Tiba Maungo (PT)
- Huduma za kisaikolojia/ushauri nasaha
- Uratibu wa huduma
- Lugha ya ishara au lugha ya mikono
- Ustawi wa jamii
- Tiba ya Matamshi-Lugha
- Usafiri
- Macho
Huduma pendekezwa zinatokana na kiasi cha usaidizi unaohitajika kuisaidia familia yako kufikia matokeo/malengo mliyoandaa wakati wa kikao cha IFSP. Utoaji wa huduma hizi unapaswa kuendana na mapendeleo ya mtoto na familia yako, mtindo wa ujifunzaji, na imani za kitamaduni.
Ufafanuzi wa huduma za EI unaweza kupatikana kwenye ukurasa wa ufafanuzi.
Jinsi huduma zinavyotolewa
Wewe na timu yako mtajadili jinsi huduma za EI zitakavyotolewa. Chaguzi ni pamoja na:
- Ziara za Ana kwa Ana: Huduma za EI zinatolewa kwa ushirikiano kati ya mzazi au mlezi na mtoa huduma za EI, wakiwepo kimwili katika eneo moja, iwe ni nyumbani au mazingira ya jumuiya. Hii ni njia ya kawaida ya kutoa huduma za EI.
- Ziara za video mbashara: Huduma za EI zinatolewa kupitia Intaneti kwenye kompyuta au tableti (k.m., iPad), jambo linaloiwezesha familia yako kushirikiana na mtoa huduma katika wakati halisi.
- Mashauriano kupitia simu: Huduma za EI zinatolewa na mtoa huduma za EI katika wakati halisi kwa njia ya simu lakini bila video. Hii ni njia ya muda mfupi tu ya kupokea huduma.
- Mseto: Huduma za EI zinatolewa kwa mchanganyiko wa ziara za ana kwa ana, ziara za video mbashara, na mashauriano kupitia simu. Hii huzipa familia uwezo wa kuitikia wasiwasi wa kiafya wa mtoto/kaya na vipaumbele vingine vya familia vinavyoweza kusababisha ziara za EI kusitishwa.
- Huduma nyingi zinaweza kutolewa vizuri kupitia ziara za video za moja kwa moja na watoa huduma wakichunguza ushirikiano kati ya mzazi na mtoto na kutoa maoni kuhusu ushirikiano huo. Mtoa huduma wako anaweza kubuni shughuli au sehemu ya shughuli za kila siku na kukuomba uchunguze. Kisha utaambiwa ujaribu mkakati au shughuli hiyo na mtoto wako.
Nani Anatoa Huduma?
Huduma zinatolewa na wafanyakazi wenye ujuzi ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:
- Waelimishaji maalum (wataalamu wa masuala ya ukuaji)
- Wataalamu wa matatizo ya kusikia na matamshi/lugha
- Wataalamu wa tiba ya shughuli za kawaida
- Wataalamu wa tiba ya mwili
- Wanasaikolojia
- Watoa huduma za jamii
- Wauguzi
- Wataalamu wa lishe
- Wataalamu wa tiba ya familia
- Wataalamu wa mwelekeo na kutembea
- Madaktari wa watoto na madaktari wengine
- Madaktari wa macho
Hatua Inayofuata: Mapitio wa IFSP

