Afua za Awali ni programu ya jimbo zima ambayo inatoa usaidizi na huduma kwa familia ili kuwasaidia watoto wao walio chini ya miaka 3 kufikia hatua muhimu za ukuaji.
Mtu yeyote anaweza kumrufaa mtoto katika programu ya EI. Ushiriki ni hiari.
Uelekezaji
Mtu yeyote anaweza kuelekeza mtoto kupokea msaada wa mapema – wazazi, madaktari, watoa huduma wengine wa afya, watoa huduma za watoto, mashirika ya huduma za jamii, mipango ya mafunzo ya mapema, n.k. Baada ya uelekezaji, ni jukumu la familia kuamua iwapo inataka kushiriki.
Wapigie ofisi yako mahalia ya Child and Family Connections (CFC) kuomba tathmini ya ukuaji. Kupata ofisi yako mahalia, piga (800) 843-6154. Familia zinapaswa kupokea simu ndani ya siku mbili za kazi.
Uandikishaji
Utakutana na Mratibu wa Huduma ili kuzungumza kuhusu wasiwasi wako kuhusu mtoto wako. Utaombwa kusaini fomu za ridhaa na kukubali kwamba mratibu wa huduma anaweza kushirikisha taarifa kuhusu mtoto wako kwa timu ambayo itampima na kumtathmini mtoto wako na inayoweza kukusaidia
kupanga huduma za EI.
Utathmini
Uelewa wako huu unakufanya kuwa mshirika muhimu kwenye timu ya mtoto wako. Timu itampima na kumtathmini mtoto wako katika maeneo yote matano ya ukuaji. Baada ya tathmini kukamilika, utaarifiwa na CFC kama mtoto wako ana ustahiki.
Ustahiki
Mtoto wako mdogo (mchanga hadi miezi 36) ana ustahiki wa huduma kupitia programu ya EI Illinois ikiwa
- ana uchelewaji wa 30% katika angalau eneo au nyanja moja ya ukuaji, au
- ana ugonjwa unaojulikana kusababisha tatizo la uchelewaji wa kukua au ulemavu, au
- yupo katika hatari kubwa ya uchelewaji mkubwa wa kukua.
Tayarisha IFSP
Mnapaswa kufanya kikao cha kuandaa IFSP mapema iwezekanavyo ila isizidi siku 45 tangu mtoto wako kupewa rufaa kwenda programu ya EI. Hakuna tozo wala gharama za kuandaa mpango.
Huduma
Afua za awali huduma lazima zianze ndani ya siku 30 baada ya kusaini IFSP na zinapaswa kutolewa katika mazingira halisi ya mtoto. Wakati wa ziara za EI mtoa huduma anaweza kukusaidia kuingiliana na mtoto wako ili kusaidia ukuaji wake.
Mapitio IFSP
Wewe na timu yako ya IFSP mtapitia maendeleo ya mtoto kila baada ya miezi sita na kuboresha mpango angalau mara moja kwa mwaka. Mahitaji yako yakibadilika, wewe na timu yako mnaweza kukutana mara nyingi zaidi ili kuubadili mpango kadri itakavyohitajika.
Mpito
Mtoto wako anaweza kuondoka kwenye programu ya EI baada ya ukuaji wake kuimarika na matokeo ya mtoto wako kuwa yamefikiwa. Vinginevyo, mtoto wako anaweza kubaki katika programu ya EI hadi afikishe miaka mitatu, au huduma za ziada zikiwa chaguo kwa mtoto.
Nyenzo Muhimu za Kuingilia Mapema
Illinois Early Intervention Clearinghouse mara kwa mara hutayarisha hati za vidokezo vya kusaidia familia na watoa huduma kuelewa utaratibu wa EI.
- Hati za vidokezo vya msingi vya EI zina maelezo ya kusaidia familia kuelewa huduma zake za EI kutoka kwa utathmini hadi kwa mabadiliko na kila kitu kilichomo. (kwa Kiingereza)
- Hati za kila siku za vidokezo vya EI hutoa mawazo ya kuchangamsha na rahisi ya kusaidia familia kutumia matokeo ya EI katika shughuli za kawaida za kila siku.
- Hati za vidokezo vya ukuaji wa mtoto zinatoa maelezo kuhusu ukuaji wa watoto wadogo. (kwa Kiingereza)
- Hati za vidokezo vya Ziara ya Video ya Moja kwa Moja zinaeleza ziara za video za moja kwa moja na jinsi familia na watoa huduma wanaweza kushirikiana kupitia mtandaoni. (kwa Kiingereza)
Mpango wa Msaada wa Mapema wa Illinois: Mwongozo wa Familia una maelezo kuhusu Mpango wa Msaada wa Mapema wa Illinois (EI, Early Intervention), kwa nini huduma za EI ni muhimu, jinsi ya kutambua iwapo mtoto wako anastahili kupokea huduma za mpango wa EI, kuanza na kuacha kupokea huduma za EI, haki zako za kisheria na maswali yanayoulizwa sana na familia.
Mchakato wa Msaada wa Mapema huzipa familia maswali ya kutafakari na mada za kujadili katika utaratibu wote wa EI. (kwa Kiingereza)
Pata maelezo zaidi kuhusu on uanza Kupokea Msaada wa Mapema:


